• Twitter
  • Facebook
  • Instagram
Isaack Zake
  • Home
  • Kuhusu Mimi
  • Huduma
  • Vitabu
  • ULIZA
  • Shop
  • Blog
  • Mawasiliano
  • Search
  • Menu Menu
ELIMU

AES.10. Changamoto za Mfumo rasmi wa Elimu – Masomo usiyoyahitaji

Utangulizi

Karibu sana ndugu msomaji wetu. Katika makala iliyopita  tulijifunza juu tuliangalia changamoto Ushindani usio na tija. Leo hii tunaangalia juu ya changamoto ya Masomo Usiyoyahitaji. Karibu sana.

Tunaendelea kuzichambua changamoto ambazo zipo ndani ya mfumo wa elimu na jinsi zinavyoweza kuathiri wanafunzi ambao tunatarajia kuwa wazalishaji katika taifa lolote ili kujiletea maendeleo.

3. Changamoto ya Masomo Usiyoyahitaji

Kuna siku moja niliamua kutafakari juu ya safari yangu ya masomo tangu awali mpaka sasa. Nilijaribu kuorodhesha masomo mbalimbali niliyosoma angalau kuanzia kidato cha kwanza. Nilishangazwa na msururu wa masomo ambayo hata mimi sikudhani kama niliwahi kusoma na kufanya vizuri. Lakini leo hii masomo yale ni kiasi kidogo sana ninayatumia maarifa yake kwenye maisha yangu.

Hali hii ipo kwa watu wengi au mfumo wetu unatuandaa hivyo. Wewe peke yako jaribu kuangalia idadi ya masomo au ‘course’ ulizosoma tangu sekondari tu mpaka sasa uone ni kwa kiasi gani masomo haya unayatumia kwenye maisha yako ya kila siku.

Tunayo haja mara kwa mara kuitafakari hasa maana ya elimu ambayo niliwahi kuiandika kwenye mfululizo wa makala hizi. Kwa kurejea ningependa kuinukuu

‘ni kitendo au mchakato wa kupata jumla ya maarifa, kukua kwa uwezo wa kufikiri au kuamua na kujiandaa binafsi kimaisha’

Kwa kifupi elimu unaweza kusema ni mfumo wa taarifa unazozihitaji wewe binafsi ili kupata maarifa yatakayokusaidia katika safari yako binafsi ya kimaisha. Msisitizo wa tafsiri hii ni kuwa elimu ili iwe imefikia lengo lake ni lazima ikunufaishe wewe binafsi ili na wewe uweze kuinufaisha jamii. Hatahivyo, kwa jinsi mfumo ulivyokaa ni kama tunabahatisha juu ya utoaji wa elimu ndio maana tunalundika masomo mengi kwa wanafunzi ili yumkini kuna kitu ataambulia ili kimsaidie. Hapa tunakosea sana na kupoteza muda.

Tunaweza kuona nyakati hizi hasa shule za msingi ‘english academy’ zinavyorundika masomo mengi kwa watoto wadogo. Unaweza kuona mtoto wa chini ya darasa la 3 ana masomo takribani 10. Ni kweli tunaweza kusema watoto wana uwezo mzuri wa kujifunza lakini mtazamo wangu wanapaswa kujifunza vitu vicheche kwa undani zaidi. Mfano ningependelea mtoto wa chini ya darasa la 3 kujifunza zaidi juu ya KUSOMA, KUANDIKA na KUHESABU. Nguvu nyingine ipelekwe katika kuvumbua vipaji vyake ili vije kumsaidia zaidi.

Nikupe changamoto ndugu msomaji, kagua vyeti vyako angalia kozi au masomo uliyosoma katika ngazi za sekondari au chuo ni masomo mangapi kwa sasa unaweza kuyatumia kuleta manufaa kwako na kwa jamii?

Nikuhakikishie unaweza kukuta ni chini ya 5% ya kile ulichojifunza darasani kwa miaka yote ndicho unatumia kwa sasa. Tutafute namna ya kuwasidia watoto na vijana wetu kujifunza kwa ajili ya safari za maisha yao binafsi na si kile mitaala inachotaka kuwalisha.

 ‘Mungu ibariki Afrika’

Isaack Zake

Wakili, Mwalimu na Mshauri

Wasiliana na Isaack Zake kwa barua pepe info@isaackzake.co.tz au kwa simu 0713 888 040 kwa ushauri na mafundisho.

Share this:

  • Click to share on LinkedIn (Opens in new window) LinkedIn
  • Click to share on X (Opens in new window) X
  • Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
  • Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
  • Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
June 23, 2020/2 Comments/by Isaack Zake
Share this entry
  • Share on Facebook
  • Share on Twitter
  • Share on WhatsApp
  • Share on LinkedIn
  • Share by Mail
https://isaackzake.co.tz/wp-content/uploads/2020/02/zake-2.png 0 0 Isaack Zake https://isaackzake.co.tz/wp-content/uploads/2020/02/zake-2.png Isaack Zake2020-06-23 05:35:472020-06-23 05:35:53AES.10. Changamoto za Mfumo rasmi wa Elimu – Masomo usiyoyahitaji
2 replies
  1. SangaVictor
    SangaVictor says:
    June 24, 2020 at 7:07 am

    Ni ukweli usiopingika kabisa, nimejaribu kuvuta picha kidogo tu na kuona kuwa tumejazwa vitu visivyo na maana na ktk mfumo huo pia tunaoutumia ndio unaoperekea watu kuchagua kusomea vitu kwa kubahatisha mean mbali kabisa na ndoto yake…. Tunajazwa story za kinjekitile ngwale stor za kina mabara the farmer sijui kina Three suitors one husband until now sijui ndayatumia wap haya!? In fact we need changes..????

    Reply
    • Isaack Zake
      Isaack Zake says:
      July 2, 2020 at 10:05 pm

      Karibu sana Victor ni kweli tunayo changamoto kubwa ya mfumo huu lakini lipo tumaini kwa kizazi hiki kama watatumia fursa kubwa ya teknolojia iliyopo kujifunza vitu wanavyotaka.

      Reply

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply to Isaack Zake Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

MAKUNDI YA MAKALA

  • ELIMU (20)
  • FAMILIA (2)
  • KIPAJI CHANGU (14)
  • KUSUDI LA MAISHA (13)
  • MAANA YA KAZI (17)
  • MAKALA (2)
  • NENO LA MUNGU (8)
  • SPIRITUAL FOOD (55)

MAKALA MPYA

  • Day.55. Spiritual Food: Je, ulipo kuna maneno ya uzima wa milele? March 26, 2022
  • Day.54. Spiritual Food: Je, unataka kuondoka? March 24, 2022
  • Day.53. Spiritual Food: Je umekwazwa na kitu gani maishani? January 15, 2022
  • AES.20. Upimaji ni rahisi kuwa na udanganyifu November 8, 2021
  • Day.52. Spiritual Food: Twamwendea Bwana Yesu kwa Neema October 18, 2021

Kuhusu | Vitabu | Mawasiliano

© 2020 Isaack Zake. All Rights Reserved

Day.28. Spiritual Food: Kubali Neno la Yesu siku zote Day.29. Spiritual Food: Wewe ni nani?
Scroll to top