
Karibu sana ndugu msomaji wa makala mbalimbali katika mtandao huu wa isaackzake. Tunamshukuru Mungu sana kwa nafasi aliyotupa tena kukutana na wewe msomaji kwa njia ya makala hizi.
Katika makala zilizotangulia tumejifunza juu ya maana ya kusudi na hatua ambazo zinapaswa kuchukuliwa na mtu ili kufahamu kusudi la maisha yake. Leo tunaanza kuangalia kanuni za msingi sana kuhusu kusudi. Kanini hizi si za muda bali zilikuwepo, zipo na zitaendelea kuwepo. Sifa ya kanuni hizi ni kwamba hazibadiliki. Kila mmoja wetu akizitambua na kuziishi anaweza kufanikiwa kulijua kusudi la maisha yake na kuweza kulitumikia kwa kipindi chote atakachojaliwa kuwepo hapa duniani. Karibu tujifunze Kanuni ya 1 ya Kusudi.
Mungu ni wa Kusudi
Ndivyo ilivyo ya kwamba Mungu aliyeziumba Mbingu na Nchi ni Mungu wa Kusudi. Hii ina maana utendaji wake wote unasukumwa na makusudi yaliyopo moyoni mwake na si vinginevyo. Mungu huwa hafanyi vitu kwa ushawishi wa kitu au viumbe vyake bali hufanya vitu kulingana na kusudi lake tangu milele.
Makusudi ya moyo wake ndiyo yanamsukuma kufanya kile anachofanya kila siku. Kama tunaweza kujifunza na kuweza kupata kujua kile tunachopaswa kufanya katika maisha yetu ni dhahiri tunapaswa kujifunza juu ya Mungu wa Kusudi.
Tunaweza kuliona hili kulingana na kile maandiko yanachoeleza
BWANA wa majeshi ameapa, akisema, Hakika yangu kama vile nilivyoazimia, ndivyo itakavyokuwa; na kama nilivyokusudia, ndivyo itakavyotokea; Isa.14:24
Shauri la BWANA lasimama milele, makusudi ya moyo wake vizazi na vizazi’ Zab.33:11
Tunaweza kuona katika maandiko haya dharihi ya kuwa Mungu husimamia makusudi yake siku zote, kama alivyokusudia ndivyo itakavyokuwa siku zote.
Kama tunataka kujua kusudi la maisha yetu ni lazima tuwe na mtazamo huu kuhusiana na Mungu wa Kusudi ya kwamba Yeye habadilishwi na mwenendo wetu au matamanio yetu bali tukijifunza kuhusiana na kusudi lake basi kwa hakika tutalifikia na kujifunza zaidi kutoka kwake.
Isaack Zake
Wakili, Mwandishi na Mshauri
Isaack Zake ni wakili wa kujitegemea na mshauri katika masuala mbalimbali ya sheria za kazi na rasilimali watu, ndoa na sheria za ardhi na mikataba. Isaack Zake ni mwanzilishi wa mtandao wa kutoa elimu, ushauri na msaada wa kisheria wa www.ulizasheria.co.tz ni mwandishi wa vitabu na makala mbalimbali kwenye nyanja za kisheria, kijamii, kiuchumi na kiroho na mwalimu wa makundi mbalimbali ya kijamii kupitia mtandao wa www.isaackzake.co.tz . Isaack Zake pia ni Mkurugenzi wa Idara ya Sheria na Uhusiano wa chama cha Waajiri TAACIME – www.taacime.co.tz.
Wasiliana na Isaack Zake kwa barua pepe info@isaackzake.co.tz au kwa simu 0713 888 040 kwa ushauri na mafundisho. Mungu akubariki sana.
Leave a Reply
Want to join the discussion?Feel free to contribute!