KUHUSU ISAACK ZAKE

Isaack Zake ni wakili wa kujitegemea na mshauri katika masuala mbalimbali ya sheria za kazi na rasilimali watu, ndoa na sheria za ardhi na mikataba. Isaack Zake ni mwanzilishi wa mtandao wa kutoa elimu, ushauri na msaada wa kisheria wa www.ulizasheria.co.tz ni mwandishi wa vitabu na makala mbalimbali kwenye nyanja za kisheria, kijamii, kiuchumi na kiroho na mwalimu wa makundi mbalimbali ya kijamii. Isaack Zake pia ni Mkurugenzi wa Idara ya Sheria na Uhusiano wa chama cha Waajiri TAACIME – www.taacime.co.tz

Kiu kubwa ya Isaack Zake ni kujenga rasilimali watu kimaarifa ili kuwawezesha kutimiza makusudi ya maisha yao kutumia vipawa, maarifa na ujuzi  waliyonao.

Ni imani ya Isaack Zake ya kuwa kila mtu anayo kazi ndani yake ila changamoto kubwa ni kuijua ni kazi ya aina gani ya kuifanya. Katika mazingira ya sasa nchi za Afrika zimekumbwa na tatizo kubwa la ukosefu wa ajira hasa kwa kundi kubwa la vijana. Hali hii imeendelea kusababisha matatizo makubwa ya UJINGA, UMASIKINI na MARADHI kuendelea kukithiri siku hadi siku.

Kazi kubwa ya mtandao huu wa Isaack Zake ni kushughulikia tatizo kubwa la UJINGA kwa kutoa maarifa, ujuzi na hekima ambazo zinaweza kutumiwa na kizazi hiki kwa kukabiliana na changamoto za karne ya 21. Endapo jamii ya kiafrika itapata MAARIFA sahihi na kuyaweka kwenye vitendo basi ni rahisi kwa kila mwafrika kushughulikia suala la umasikini na maradhi.

Mtandao huu ni mahsusi kwa watu wa rika zote na utakuwa na utaratibu wa kutoa mafunzo.

Karibu sana ushirikiane na Isaack Zake katika kubadilisha fikra zako binafsi ili kutoa mchango wako kwa Tanzania, Bara la Afrika na dunia kwa ujumla.

‘Wewe ni wa pekee sana na unacho kitu cha kipekee ambacho hakuna mwengine aliyenacho hapa duniani, hivyo ungana na isaack zake katika kujenga uwezo wa kutoa kitu hicho kwa ajili ya dunia’

NAFASI ZA UONGOZI

  • Mjumbe wa Serikali ya Wanafunzi – Mzumbe Sekondari – 2004 – 2005
  • Mbunge wa Kuchaguliwa Serikali ya Wanafunzi Tumanini University – Iringa University College – 2008
  • Mwanzilishi na Katibu mkuu wa ‘Community Legal Service Centre’ 2009 – 2011
  • Mwanzilishi wa Ofisi ya Uwakili Zake Advocates 2012 – mpaka sasa.
  • Mwanzilishi wa ‘Creative Tz’ – 2013
  • Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana KKKT – Kinyerezi Mtaa wa Kibaga 2016 – 2018
  • Katibu wa chama cha Kibaga Brothers 2017 – Mpaka sasa.
  • Mwanzilishi wa mtandao wa Uliza Sheria – 2018
  • Mkurugenzi wa Idara ya Sheria na Uhusiano TAACIME – 2019

TUZO NA VITABU

TUZO

  • Mshindi wa Pili wa uandishi wa Insha – Kuleana NGO – 2004
  • Tuzo ya Uongozi bora Serikali ya Wanafunzi Mzumbe Sekondari – 2006
  • Tuzo ya Ubunifu Mzumbe Sekondari – 2006

Uandishi wa Vitabu

  1. Tathmini ya Ndoa Miaka 5 Makosa 50
  2. Nguzo 12 za Uanafunzi
  3. Maana ya Kazi
  4. Je, wewe ni Mwajiri au Mwajiriwa?
  5. Viwango vya Ajira

Kupata Vitabu Hivi Bonyeza Link hii www.isaackzake.co.tz/vitabu