
Utangulizi
Karibu tena ndugu msomaji katika mfululizo wa makala hizi za kujifunza juu ya maana ya kazi kwa lengo la kuboresha maisha yetu kila siku na kusaidia watu wengi ambao wanapaswa kufanya kazi ili kuingia kazini.
Katika makala zilizotangulia tumeangalia tofauti za kimsingi baina ya ‘kazi’ na ‘ajira’ambazo zimeelezwa kwa undani zaidi. Sasa tuangalie changamoto zinazokumba sekta ya ajira ili kutuwezesha kubadili mtazamo wetu kutoka katika kutegemea ‘ajira’ na kuanza kufanya ‘kazi’ kwa lengo la kuboresha maisha yetu.
Kama tunavyosema ya kuwa mtu, jamii au taifa halina changamoto ya ukosefu wa ‘kazi’ bali kuna changamoto ya ukosefu wa ‘ajira’ hii ni kwa sababu kila mtu anayo kazi ya kufanya ila si kila mtu ana ajira.
Zipo changamoto kadhaa ambazo zinaikumba sekta ya ajira na kusababisha ongezeko kubwa sana la watu wasio na ajira. Leo tunaangalia changamoto ya kiuchumi.
Hali ya kiuchumi ya mtu binafsi au jamii au taifa au dunia inaweza kwa sehemu kubwa sana kuathiri hali ya kiajira ya eneo au mtu. Kama uchumi wa kijamii au taifa hautakuwa mzuri basi tunatarajia ongezeko kubwa la ukosefu wa ajira. Hivi karibuni tumeshuhudia ongezeko kubwa sana la ukosefu wa ajira kutokana na madhara ya ugonjwa wa Corona ulioikumba dunia yote. Watu wengi wamepoteza ajira zao na zimeendelea kupotea zaidi kwa sababu ya madhara haya.
Hivyobasi, ni muhimu sana kwetu kubadili mtazamo wetu na hasa vijana tunaowaandaa kutokufikiria juu ya ‘ajira’ bali kujifunza juu ya kile kilichopo ndani yao yaani ‘kazi’ ili waweze kuifaa jamii na dunia kwa ujumla. Hii ni kwa sababu suala la uchumi linabadilika mara kwa mara na kuhatarisha ajira za watu lakini mtu mwenye kutenda kazi iliyo ndani yake bado ana uwezo wa kubadilika na kuongeza ufanisi zaidi hata katika hali ngumu za kiuchumi.
Asiyetaka kufanya kazi na asile…’
Isaack Zake
Wakili, Mwalimu na Mshauri
Wasiliana na Isaack Zake kwa barua pepe info@isaackzake.co.tz au kwa simu 0713 888 040 kwa ushauri na mafundisho.
Leave a Reply
Want to join the discussion?Feel free to contribute!