
Utangulizi
Karibu tena ndugu msomaji katika mfululizo wa makala hizi za kujifunza juu ya maana ya kazi kwa lengo la kuboresha maisha yetu kila siku na kusaidia watu wengi ambao wanapaswa kufanya kazi ili kuingia kazini.
Katika mfululizo wa makala za tofauti ya kazi na ajira tumeanza kwa kuangalia maana ya neno kazi katika makala iliyotangulia. Leo tunaangalia maana ya neno ‘ajira’ ili kuichambua misingi muhimu wa kutofautisha kati ya neno ‘kazi’ na ‘ajira’ karibu sana.
Maana ya Ajira
Neno ajira kwa tafsiri ya kiingereza lina maana ya neno ‘job’. Kwenye kamusi ya kiingereza neno ‘job’ lina maana ya ‘Is regular and official activity that you do and receive money/salary for your activity. Kwa tafsiri isiyo rasmi tunaweza kusema ajira ni shughuli inayofanyika mara kwa mara kwa ajili ya kupata fedha kama malipo ya shughuli husika. Hii ina maana ya kuwa mtu anayefanya shughuli kwa maana ya ajira anaifanya kwa lengo au kusudi la kupata fedha.
Kwa mantiki ya maana hii ya ajira na kwa jinsi ya neno ajira lilivyo msingi mkuu wa ajira ni kusudia la kupata fedha. Ndio maana fedha inayopatikana kutokana na ajira huitwa ujira.
Katika neno ajira tunaweza kujifunza vipengele muhimu;
- Shughuli ya mara kwa mara au inayotambulika; ajira inahusisha shughuli au jambo ambalo mtu hulifanya kwa kawaida au mara kwa mara. Shughuli hii huwa inatambuliwa na mamlaka au watu wanaomzunguka huyo anayeifanya na kumtambua kutokana na nafasi aliyonayo kwa mujibu wa shughuli anayoifanya.
- Fedha; lengo au kusudi la kutenda shughuli hiyo ni kupata fedha au malipo ya fedha yanayojulikana kama ujira mara baada ya kutenda shughuli hiyo.
Kama tulivyoona katika tafsiri ya maneno haya mawili yaani kazi na ajira kwa sehemu kubwa yote yanashabihiana kwa sababu yanahusisha ‘utendaji wa jambo au shughuli’ tofauti kubwa baina ya maneno haya ipo kwenye malengo na matokeo yake.
Neno kazi ni pana zaidi ya neno ajira tunaweza kusema ndani ya kazi unaweza kukuta ajira endapo kazi hiyo ni shughuli ambayo inakupa matokeo ya kipato. Hata hivyo unaweza kufanya kazi pasipo kuwa na kipato. Hii inahusisha sababu ya kufanya kazi kuwa kubwa zaidi ya kupata fedha kama ujira.
Mfano mtu anafanya shughuli za kujitolea katika jamii inamaanisha huyu ana kazi anaifanya yenye malengo ya kutoa uwezo wake na nguvu zake kwa manufaa ya kijamii pasipo kupata fedha kama ujira.
Pia watoto au vijana wetu wanaofanya shughuli za nyumbani kama kupika au kufua au kuchota maji n.k hizi zote ni kazi lakini hazina uhusiano wa kuwaingizia wao kipato kama ujira.
Baada ya kuona tofauti hizi za kimsingi kati ya neno ‘kazi’ na ‘ajira’ fuatilia makala zinazoendelea ili kujifunza zaidi tofauti baina ya maneno haya.
Asiyetaka kufanya kazi na asile…’
Isaack Zake
Wakili, Mwalimu na Mshauri
Wasiliana na Isaack Zake kwa barua pepe info@isaackzake.co.tz au kwa simu 0713 888 040 kwa ushauri na mafundisho.
Leave a Reply
Want to join the discussion?Feel free to contribute!