Katika kushughulikia changamoto ya kimaarifa, mtandao huu unatoa huduma zifuatazo
1. Elimu (Knowledge)
Katika kutoa elimu au maarifa mbalimbali mtandao huu utahusisha
- Makala mbalimbali za kiroho, kijamii, kiuchumi
- Vitabu mbalimbali
- Semina na makongamano
2. Ushauri (Consultancy and Counselling)
Katika ushauri mtandao huu utaweka utaratibu wa wasomaji na wafuatiliaji kupata ushauri katika maeneo mbalimbali ya kimaarifa.
3. Usimamizi wa vipaji na mawazo ya kibiashara (Talent and Business ideas management)
Kila mmoja ana uwezo wa asili ndani yake yaani kipaji au vipawa, hivyo mtandao huu utahusika na kuelimisha namna ya kugundua kipaji na kukiendeleza na kuwezesha usimamizi wa mawazo ya uvumbuzi na kibiashara.
4. Mfumo Mbadala wa Elimu (Alternative Education System)
Maelezo
Moja ya changamoto kubwa sana za ukosefu wa maendeleo katika nchi za Afrika ni aina ya mfumo wa elimu tuliorithi kutoka kwa wakoloni. Mfumo huu umekuwa na changamoto ambazo kwa kiasi kikubwa umeua uwezo wa uvumbuzi na matumizi ya vipaji vya watu binafsi. Mtandao wa Isaack Zake utahusisha namna ya kutoa maarifa sahihi yanayoambatana na changamoto za karne ya 21 ili watu waweze kufanya kazi zao na kuunda ajira zaidi.
Mfumo huu utahusisha maeneo makuu 5
- Maarifa ya kiroho (Spiritual Knowledge)
- Maarifa binafsi (Self knowledge)
- Maarifa ya ujuzi kimaisha (Life Skills)
- Maarifa ya mifano ya watu (Personal experience)
- Maarifa ya kimfumo (Formal knowledge)