
Utangulizi
Karibu sana ndugu yangu msomaji wa mtandao huu wa isaack zake. Katika kipengele cha maarifa ya kiroho ya Uliza Neno tunakwenda kujifunza mambo mbalimbali yanayoanishwa na neno la Mungu kwa lengo la kutusaidia utu wetu katika safari na majukumu tuliyonayo hapa duniani siku kwa siku. Katika somo lililopita tuliendelea kujifunza habari za kusudi la chakula. Makala iliyopita tulijifunza habari za Gharama ya Chakula cha kiroho. Leo tunajibu swali la ‘Je, ni chakula gani kinakushughulisha?. Karibu sana.
‘Msikitendee kazi chakula chenye kuharibika, bali chakula kidumucho hata uzima wa milele; ambacho Mwana wa Adamu atawapa, kwa sababu uyo ndiye alitiwa muhuri na Baba yaani Mungu’ Yn.6:27
Ujumbe huu ulionenwa na Bwana Yesu akitoa maelekezo kwa wafuasi wake juu ya aina za chakula na matokeo ya kila chakula katika maisha ya mtu
Mambo ya kujifunza
- Sisi sote tunakubaliana ya kwamba mfumo wa maisha ya mwanadamu ni lazima ale chakula ili aishi. Na kwamba vipo vyakula kwa ajili ya utu wa nje na vipo kwa ajili ya utu wa ndani yaani roho na nafsi.
- Je, aina gani ya chakula inayotuamsha kila siku asubuhi kukitafuta? Majibu yetu ni dhahiri ya kuwa shughuli zinazotuhangaisha kila siku ni kuhakikisha tunapata chakula cha miili yetu.
- Tunakwenda kazini, tunajifunza vitu vingi, tunafanya biashara, vibarua kwa lengo la kuhakikisha tunapata mkate wa kila siku. Huo ndio mfumo wa maisha yetu kila siku.
- Bwana Yesu anatupa kipaombele sahihi juu ya utendaji kazi wetu, ya kuwa tusitendee kazi chakula kinachoharibika. Hii ina maana kile ambacho tunakula kwa miili yetu ni kwa kitambo tu kwani mara baada ya kula katika mwili mwisho wake ni uharibifu.
- Chakula cha mwili hakipaswi kuwa kipaombele chetu cha kwanza kwani hakina uwezo wa kudumu zaidi ya maisha ya mwili.
- Tumesikia mafundisho mengi ya kuwa hata kwa sehemu kubwa ya maradhi yanayowakuta wanadamu nyakati hizi ni matokeo ya tabia za ulaji. Hatujui kitu gani cha kula wala hatufuati kanuni za asili za ulaji. Maisha ya ulaji yamechangia sana magonjwa makubwa na hata kupelekea vifo vya wapendwa wetu.
- Dunia imepoteza watu wengi sana na mchango wao kutokana na chakula. Hii ni dhahiri ya kuwa maisha ya ulaji yanachangia sana uharibifu wa miili yetu.
- Hatahivyo haimaanishi hatupaswi kula katika mwili, ila tunapaswa kujua ni nini hasa kipaombele cha Mungu katika maisha yetu ili kujua nafasi ya chakula cha mwili.
Mungu mwenyewe aliyetuita ni mwaminifu, naye atafanya katika Jina la Mwana wake Mpendwa Yesu Kristo, Bwana na Mwokozi wa maisha yetu. Amen
‘Utupe leo riziki yetu’
Isaack Zake
Wakili, Mwalimu na Mshauri
Isaack Zake ni wakili wa kujitegemea na mshauri katika masuala mbalimbali ya sheria za kazi na rasilimali watu, ndoa na sheria za ardhi na mikataba. Isaack Zake ni mwanzilishi wa mtandao wa kutoa elimu, ushauri na msaada wa kisheria wa www.ulizasheria.co.tz ni mwandishi wa vitabu na makala mbalimbali kwenye nyanja za kisheria, kijamii, kiuchumi na kiroho na mwalimu wa makundi mbalimbali ya kijamii kupitia mtandao wa www.isaackzake.co.tz . Isaack Zake pia ni Mkurugenzi wa Idara ya Sheria na Uhusiano wa chama cha Waajiri TAACIME – www.taacime.co.tz.
Wasiliana na Isaack Zake kwa barua pepe info@isaackzake.co.tz au kwa simu 0713 888 040 kwa ushauri na mafundisho. Mungu akubariki sana.
Leave a Reply
Want to join the discussion?Feel free to contribute!