• Twitter
  • Facebook
  • Instagram
Isaack Zake
  • Home
  • Kuhusu Mimi
  • Huduma
  • Vitabu
  • ULIZA
  • Shop
  • Blog
  • Mawasiliano
  • Search
  • Menu Menu
SPIRITUAL FOOD

Day.45. Spiritual Food: Chakula cha kweli

Utangulizi

Karibu sana ndugu yangu msomaji ni siku nyingine tena tumepewa na Mungu kwa ajili ya kuendelea kujifunza zaidi misingi ya chakula cha kiroho ili kutuwezesha kufanya mapenzi yake na kumtumikia kwa furaha na upendo siku ya leo.

‘Kwa maana mwili wangu ni chakula cha kweli, na damu yangu ni kinywaji cha kweli’ Yn.6:55

Mambo ya kujifunza

  • Si kila chakula anachokula mwanadamu ni cha kumsaidia katika kuboresha maisha yake. Wapo watu wengi wanapata maradhi na hata kupoteza maisha kwa kula vitu ambavyo havina msaada katika miili yao.

  • Wapo watu wanakula sumu au wanakunywa sumu kwa lengo la kukatisha maisha yao au kuleta madhara katika utu wao.

  • Kama kuna kitu kinaweza kukatisha maisha ya mwanadamu kwa haraka ni kula kitu ambacho ni kinyume na mfumo wa kawaida wa maisha.

  • Kama kipo chakula cha kweli na kinywaji cha kweli ina maana kipo chakula na kinywaji cha uongo. Je, mimi na wewe tunakula nini au tunakunywa nini siku ya leo?

  • Bwana Yesu anatuambia ya kuwa mwili wake ndio chakula cha kweli na damu yake ndio kinywaji cha kweli. Tukitaka uhakika wa maisha yetu na usalama wetu kila siku tunapaswa kukitafuta chakula cha kweli na kinywaji cha kweli. Tuna sababu ya kupata neno la Kristo kwa ajili yetu ili kutuongoza na kutuwezesha kuishi katika makusudi ya Mungu. Halikadhalika tukitaka kusafishwa na dhambi yote na kuwa na haki mbele zake tunahitaji Damu ya Yesu Kristo kututakasa kila siku.

  • Si kila kitu kinafaa kuwa chakula kwetu au kinywaji chetu bali kile ambacho Yesu Kristo anatuambia kila iitwapo leo.

MAOMBI LEO

Ndugu yangu ikiwa ndani yako unashuhudiwa bado huna uhakika wa maisha yako na kumjua Mungu ipasavyo, ujue unahitaji ufahamu huo kupitia uzima wa Mungu kuingia ndani yako. Karibu ufuatane nami katika kuomba maombi haya ili uzima wa Mungu ukae ndani yako sasa;

‘Ee Mungu Baba ninakushukuru kwa neno lako la uzima, asante kwa sadaka ya Mwana wako Yesu Kristo pale msalabani kwa ajili yangu. Bwana Yesu ninakiri udhaifu wangu na wasi wasi wangu wa kupotea milele endapo nitaondoka katika maisha haya. Ninaomba unisamehe dhambi zangu zote nilizofanya na hata kuondoa asili ya dhambi ndani yangu, unitakase kwa Damu yako takatifu. Ninaomba ufute jina langu katika kitabu cha hukumu na kuliandika katika kitabu cha uzima. Ninaomba uniokoe na kunifanya upya ndani yangu kwa nguvu ya Roho Mtakatifu. Uingie ndani yangu na kuniongoza tangu sasa na hata milele’ Amen.

Ikiwa umefanya sala hii kwa imani, Mungu kwa neema yake amekurehemu na kukusamehe kabisa, hata kama umefanya dhambi yeye ameisafisha na kuisahau. Unapaswa na wewe kujisamehe na kumfuata Yesu tangu sasa.

Mungu mwenyewe aliyetuita ni mwaminifu, naye atafanya katika Jina la Mwana wake Mpendwa Yesu Kristo, Bwana na Mwokozi wa maisha yetu. Amen

 ‘Utupe leo riziki yetu’

Isaack Zake

Wakili, Mwalimu na Mshauri

Wasiliana na Isaack Zake kwa barua pepe info@isaackzake.co.tz au kwa simu 0713 888 040 kwa ushauri na mafundisho. Mungu akubariki sana

Share this:

  • Click to share on LinkedIn (Opens in new window) LinkedIn
  • Click to share on X (Opens in new window) X
  • Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
  • Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
  • Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
February 13, 2021/0 Comments/by Isaack Zake
Share this entry
  • Share on Facebook
  • Share on Twitter
  • Share on WhatsApp
  • Share on LinkedIn
  • Share by Mail
https://isaackzake.co.tz/wp-content/uploads/2020/02/zake-2.png 0 0 Isaack Zake https://isaackzake.co.tz/wp-content/uploads/2020/02/zake-2.png Isaack Zake2021-02-13 06:57:532021-02-13 06:57:56Day.45. Spiritual Food: Chakula cha kweli
0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

MAKUNDI YA MAKALA

  • ELIMU (20)
  • FAMILIA (2)
  • KIPAJI CHANGU (14)
  • KUSUDI LA MAISHA (13)
  • MAANA YA KAZI (17)
  • MAKALA (2)
  • NENO LA MUNGU (8)
  • SPIRITUAL FOOD (55)

MAKALA MPYA

  • Day.55. Spiritual Food: Je, ulipo kuna maneno ya uzima wa milele? March 26, 2022
  • Day.54. Spiritual Food: Je, unataka kuondoka? March 24, 2022
  • Day.53. Spiritual Food: Je umekwazwa na kitu gani maishani? January 15, 2022
  • AES.20. Upimaji ni rahisi kuwa na udanganyifu November 8, 2021
  • Day.52. Spiritual Food: Twamwendea Bwana Yesu kwa Neema October 18, 2021

Kuhusu | Vitabu | Mawasiliano

© 2020 Isaack Zake. All Rights Reserved

Purpose 10. Mamlaka ya Juu ilikuchagua kabla ya kuumbwa ulimwengu Kazi 17. Je ajira ni kipimo cha maisha yako?
Scroll to top