• Twitter
  • Facebook
  • Instagram
Isaack Zake
  • Home
  • Kuhusu Mimi
  • Huduma
  • Vitabu
  • ULIZA
  • Shop
  • Blog
  • Mawasiliano
  • Search
  • Menu Menu
SPIRITUAL FOOD

Day.32. Spiritual Food: Je, unajifunza kwa nani?

Utangulizi

Karibu sana ndugu yangu msomaji ni siku nyingine tena tumepewa na Mungu kwa ajili ya kuendelea kujifunza zaidi misingi ya chakula cha kiroho ili kutuwezesha kufanya mapenzi yake na kumtumikia kwa furaha na upendo siku ya leo.

‘Imeandikwa katika manabii, na wote watakuwa wamefundishwa na Mungu. Na kila asikiaye na Kujifunza kwa Mungu huja kwangu’ Yn.6:45

Mambo ya kujifunza

  • Mafundisho ni namna ya kupokezana taarifa kutoka upand mmoja kwenda mwengine kwa nia ya kujenga maarifa kwa anayepokea taarifa. Tunapozaliwa tuna upungufu kiasi Fulani cha maarifa na tunajifunza kutoka kwa wazazi, ndugu, jamaa na marafiki.

  • Kile tunachojifunza kwa sehemu kubwa kinaathiri maisha yetu kimaamuzi, kihisia na hata kifikra. Jinsi tulivyo ni matokeo ya taarifa tulizozigeuza kuwa maarifa na kuziishi kila siku.

  • Pamoja na mfumo wa maisha ya kujifunza, Mungu ametuwekea namna ya kujifunza kutoka kwake mwenyewe. Watu wengi wanahangaika kutaka kujua jinsi Mungu anavyoongea au anavyowasiliana na watu. Kwa hakika Mungu yu karibu na kila mmoja wetu kuliko hata wale tunaodhani wapo karibu yetu. Kwa Roho Mtakatifu tunaweza kuunganishwa na Mungu kila sku.

  • Je, unaamini ya kuwa Mungu anakusikia kile unachosema naye katika sala? Basi kwa imani hiyo hiyo amini ya kuwa na wewe utamsikia akisema nawe.

  • Maandiko yanasema Roho ya Mungu ndiyo imeniumba na pumzi yake mwenyezi imenipa uhai. Fikiria kama kuna kitu kilicho karibu kwa mwanadamu kama ilivyo pumzi yake. Jibu ni hakuna kilicho muhimu na karibu ya mtu zaidi ya pumzi yake. Mungu atupaye pumzi ya uhai yu karibu sana nasi.
  • Je, yale uliyojifunza katika maisha yanakupeleka kwa nani? Kama umejifunza kwa mwanadamu basi kwa hakika mafundisho hayo yatatupeleka kwao lakini kama tukiwa tumejifunza kwa Mungu tutaishi kwa mfano wake. Kama mafundisho tunayoyapokea yanatupeleka kwa Bwana Yesu basi tupo salama katika safari yetu ila yakitupeleka kwa watu tuna mashaka na safari.

MAOMBI LEO

Ikiwa ndani yako ungependa kuona ahadi ya Bwana Yesu inatimia ya kuwa usipotee milele bali upate kufufuliwa siku ya mwisho na kwamba unaona uhusiano wako kwa sasa na Bwana Yesu si sahihi na unashuhudiwa moyoni ya kuwa endapo leo ni siku yako ya mwisho kuna uwezekano wa hukumu, basi chukua hatua na kubadili mkondo wa historia yako kwa kusali pamoja name

‘Ee Mungu Baba ninakushukuru kwa neno lako la uzima, asante kwa sadaka ya Mwana wako Yesu Kristo pale msalabani kwa ajili yangu. Bwana Yesu ninakiri udhaifu wangu na wasi wasi wangu wa kupotea milele endapo nitaondoka katika maisha haya. Ninaomba unisamehe dhambi zangu zote nilizofanya na hata kuondoa asili ya dhambi ndani yangu, unitakase kwa Damu yako takatifu. Ninaomba ufute jina langu katika kitabu cha hukumu na kuliandika katika kitabu cha uzima. Ninaomba uniokoe na kunifanya upya ndani yangu kwa nguvu ya Roho Mtakatifu. Uingie ndani yangu na kuniongoza tangu sasa na hata milele’ Amen.

Ikiwa umefanya sala hii kwa imani, Mungu kwa neema yake amekurehemu na kukusamehe kabisa, hata kama umefanya dhambi yeye ameisafisha na kuisahau. Unapaswa na wewe kujisamehe na kumfuata Yesu tangu sasa.

Mungu mwenyewe aliyetuita ni mwaminifu, naye atafanya katika Jina la Mwana wake Mpendwa Yesu Kristo, Bwana na Mwokozi wa maisha yetu. Amen

 ‘Utupe leo riziki yetu’

Isaack Zake

Wakili, Mwalimu na Mshauri

Wasiliana na Isaack Zake kwa barua pepe info@isaackzake.co.tz au kwa simu 0713 888 040 kwa ushauri na mafundisho. Mungu akubariki sana.

Share this:

  • Click to share on LinkedIn (Opens in new window) LinkedIn
  • Click to share on X (Opens in new window) X
  • Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
  • Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
  • Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
July 1, 2020/0 Comments/by Isaack Zake
Share this entry
  • Share on Facebook
  • Share on Twitter
  • Share on WhatsApp
  • Share on LinkedIn
  • Share by Mail
https://isaackzake.co.tz/wp-content/uploads/2020/02/zake-2.png 0 0 Isaack Zake https://isaackzake.co.tz/wp-content/uploads/2020/02/zake-2.png Isaack Zake2020-07-01 10:03:332020-07-01 10:03:43Day.32. Spiritual Food: Je, unajifunza kwa nani?
0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

MAKUNDI YA MAKALA

  • ELIMU (20)
  • FAMILIA (2)
  • KIPAJI CHANGU (14)
  • KUSUDI LA MAISHA (13)
  • MAANA YA KAZI (17)
  • MAKALA (2)
  • NENO LA MUNGU (8)
  • SPIRITUAL FOOD (55)

MAKALA MPYA

  • Day.55. Spiritual Food: Je, ulipo kuna maneno ya uzima wa milele? March 26, 2022
  • Day.54. Spiritual Food: Je, unataka kuondoka? March 24, 2022
  • Day.53. Spiritual Food: Je umekwazwa na kitu gani maishani? January 15, 2022
  • AES.20. Upimaji ni rahisi kuwa na udanganyifu November 8, 2021
  • Day.52. Spiritual Food: Twamwendea Bwana Yesu kwa Neema October 18, 2021

Kuhusu | Vitabu | Mawasiliano

© 2020 Isaack Zake. All Rights Reserved

Kipaji.9. Changamoto ya Vipaji vingi Day.33. Spiritual Food: Je, ni nani chanzo chako cha taarifa kuhusu Mungu?
Scroll to top