Day.28. Spiritual Food: Kubali Neno la Yesu siku zote

Utangulizi
Karibu sana ndugu yangu msomaji ni siku nyingine tena tumepewa na Mungu kwa ajili ya kuendelea kujifunza zaidi misingi ya chakula cha kiroho ili kutuwezesha kufanya mapenzi yake na kumtumikia kwa furaha na upendo siku ya leo.
‘Basi Wayahudi wakamnung’unikia kwa sababu alisema, Mimi ni chakula kilichoshuka kutoka mbinguni’ Yn.6:41
Mambo ya kujifunza
- Kuna wakati tunaweza kusikia maneno ya Yesu Kristo tusiyaelewe wala kujua kile yalichobeba kwa ajili yetu. Hali hii husababisha manung’uniko ndani yetu kama kwa wayahudi.
- Yesu alikuwa anaeleza juu ya uzima wa milele kwa kila mmoja anayesikia na kukubali neno lake kama chakula. Ni mara ngapi Bwana Yesu analeta neno lake kwa ajili ya maisha yetu na kwa kutopata ufunuo wa neno hili tunaishia kulalamika na kujitenga naye?
- Jambo la msingi kwetu tukiwa na hakika na neno lake Yesu hata kama hatujakielewa alichosema tusikatae kwanza neno lake bali tumwombe atufunulie neno husika na kulikubali kwa moyo.
- Neno analosema linaweza kuonekana gumu au si tamu katika kulisikia. Lakini tunapaswa kujua yote asemayo ni kweli na amini kwa ajili yetu.
- Wengi wetu tunapenda kuchagua hata kwa chakula cha miili yetu tunaangalia vile tunavyoona ni vitamu na vinaburudisha nafsi zetu pasipo hasa kuzingatia chakula hicho kinaenda kufanya nini ndani ya miili yetu. Vivyo hivyo kwenye mambo ya kiroho watu wanachagua cha kusikia. Wanapenda kusikia kuhusu fedha, mafanikiom kubarikiwa, mahusiano n.k watu hawataki kusikia juu ya wokovu, toba, utakatifu, msamaha kwa wengine kama msingi wa injili unavyotaka.
- Mtu wa Mungu mimi na wewe tukubali kile Bwana anatuambia kila siku hata kama tunaona hakina ladha kwenye masikio yetu ni kwa ajili ya uzima wetu.
Mungu mwenyewe aliyetuita ni mwaminifu, naye atafanya katika Jina la Mwana wake Mpendwa Yesu Kristo, Bwana na Mwokozi wa maisha yetu. Amen
‘Utupe leo riziki yetu’
Isaack Zake
Wakili, Mwalimu na Mshauri
Wasiliana na Isaack Zake kwa barua pepe info@isaackzake.co.tz au kwa simu 0713 888 040 kwa ushauri na mafundisho. Mungu akubariki sana.
Leave a Reply
Want to join the discussion?Feel free to contribute!