
Utangulizi
Karibu sana ndugu yangu msomaji wa mtandao huu wa isaack zake. Katika kipengele cha maarifa ya kiroho ya Uliza Neno tunakwenda kujifunza mambo mbalimbali yanayoanishwa na neno la Mungu kwa lengo la kutusaidia utu wetu katika safari na majukumu tuliyonayo hapa duniani siku kwa siku. Ni siku nyingine tena tumepewa na Mungu kwa ajili ya kuendelea kujifunza zaidi misingi ya chakula cha kiroho ili kutuwezesha kufanya mapenzi yake na kumtumikia kwa furaha na upendo siku ya leo.
‘Basi wakamwambia sikuzote utupe chakula hiki’ Yn.6:34
Mambo ya kujifunza
- Tunajua ya kuwa hitaji muhimu kabisa katika maisha ya mwanadamu mara baada ya pumzi ni chakula. Tunaona juu ya mtazamo wa wayahudi waliokuwa wanahojiana na Bwana Yesu ni kupata chakula cha kimwili. Hali hii ikapelekea kuleta ombi kwa Bwana Yesu wapewe chakula hicho siku zote za maisha yao.
- Hali hii ya maombi ya wayahudi hawa inatupa picha ya kuwa tunahitaji chakula kila siku ili tuendelee kuishi na kama tukipata uhakika wa chakula kwa siku zote za maisha yetu tunaweza kuendelea kuishi bila wasiwasi.
- Je, mimi na wewe leo tunapeleka ombi gani kwa Bwana Yesu? Ni hitaji gani letu la msingi ambalo tunatamani BWANA atufanyie leo na siku zetu zote?
- Wenzetu waliona hitaji kubwa la kuomba kwa Bwana Yesu ni kupewa chakula kwa ajili ya miili yao sikuzote.
- Kwa jinsi tulivyojifunza tangu mfululizo huu wa mafundisho haya ni dhahiri kuwa hitaji letu la msini ni chakula kwa ajili ya roho na nafsi zetu kila siku. Chakula hiki kinapatikana bure bila gharama yoyote isipokuwa kujenga hamu na uhitaji ndani yetu kila siku.
- Tunao uhakika wa kupokea chakula hiki siku ya leo na siku zote za maisha yetu tukimwendea Bwana Yesu kwa imani ndani yetu.
- Bwana Yesu anatukumbusha uhakika huu katika neno lake akisima ‘ni nani kati yenu aliye baba, mtoto akamwomba mkate akampa jiwe? Au akamwomba samaki akampa nyoka? au yai akampa n’ge? Vivyo hivyo kama sisi tulio waovu hatuwezi kuwapa watoto wetu vitu vibaya, je si zaidi sana kwa Baba yetu wa mbinguni tumwombapo chakula cha uzima?
Mungu mwenyewe aliyetuita ni mwaminifu, naye atafanya katika Jina la Mwana wake Mpendwa Yesu Kristo, Bwana na Mwokozi wa maisha yetu. Amen
‘Utupe leo riziki yetu’
Isaack Zake
Wakili, Mwalimu na Mshauri
Isaack Zake ni wakili wa kujitegemea na mshauri katika masuala mbalimbali ya sheria za kazi na rasilimali watu, ndoa na sheria za ardhi na mikataba. Isaack Zake ni mwanzilishi wa mtandao wa kutoa elimu, ushauri na msaada wa kisheria wa www.ulizasheria.co.tz ni mwandishi wa vitabu na makala mbalimbali kwenye nyanja za kisheria, kijamii, kiuchumi na kiroho na mwalimu wa makundi mbalimbali ya kijamii kupitia mtandao wa www.isaackzake.co.tz . Isaack Zake pia ni Mkurugenzi wa Idara ya Sheria na Uhusiano wa chama cha Waajiri TAACIME – www.taacime.co.tz.
Wasiliana na Isaack Zake kwa barua pepe info@isaackzake.co.tz au kwa simu 0713 888 040 kwa ushauri na mafundisho. Mungu akubariki sana.
Leave a Reply
Want to join the discussion?Feel free to contribute!