
Utangulizi
Karibu sana ndugu yangu msomaji wa mtandao huu wa isaack zake. Katika kipengele cha maarifa ya kiroho ya Uliza Neno tunakwenda kujifunza mambo mbalimbali yanayoanishwa na neno la Mungu kwa lengo la kutusaidia utu wetu katika safari na majukumu tuliyonayo hapa duniani siku kwa siku. Katika somo lililopita tuliendelea kujifunza habari za kusudi la chakula. Makala iliyopita tuliangalia kuhusu Chakula cha Kweli. Leo tunaangalia juu ya uwepo chakula kwa ajili yak oleo.Karibu sana.
‘Kwa maana chakula cha Mungu ni kile kishukacho kutoka mbinguni na kuupa ulimwengu uzima’ Yn.6:33
Mambo ya kujifunza
- Andiko hili linazidi kuonesha juu ya msisitizo wa Bwana Yesu kwa watu wote juu ya uwepo wa chakula cha kweli. Msisitizo huu una maana ya kuwa wapo watu wengine ambao hutoa chakula ambacho si cha kweli.
- Halikadhalika tunajifunza juu ya asili ya chakula cha kweli ni kile kinachoshuka kutoka mbinguni. Chakula hiki hakitengenezwi kwa mikono ya wanadamu bali ni neno lake Mungu mwenyewe lenye kuongoza maisha ya watu.
- Pia tunajifunza ya kuwa chakula hiki kipo kwa ajili yako na kwa ajili yangu siku ya leo na kila siku. Ipo sehemu yako ya chakula ‘portion’ yako katika meza ya Bwana siku ya leo.
- Waamini wengi hutusheka tu na mahubiri ya siku za ibada iwe Jumapili au Jumamosi kutegemeana na dhehebu, lakini maandiko yanatueleza wazi ya kuwa chakula kipo kwa ajili yetu kila iitwapo leo.
- Je, mimi na wewe tunaweza kuendelea kuishi kimwili kama tutakula tu mara moja kwa juma? Nadhani jibu ni hapana hatuwezi kuendesha maisha yetu ya kimwili kwa mlo mmoja katika juma zima. Je, kwa nini tunafikiri roho na nafsi zetu zitaishi katika uzima wakati tunapanga kula kwa siku 1 ndani ya juma?
- Nyakati hizi za mifumo ya teknolojia tuna fursa kubwa ya kupata kujifunza neno la Mungu kupitia vyanzo mbalimbali kama simu, runinga, intaneti, radio, n.k Asubuhi na mapema kila siku hakikisha unapanga kuzilisha nafsi na roho yako kupitia mafundisho mbalimbali lakini pia jifunze mwenyewe kwa kusoma neno na kulitafakari.
- Fikiri juu ya Bwana Yesu kila siku anakuandalia meza ya chakula cha asubuhi, mchana na jioni lakini huonekani mezani, je hasara kubwa ni kwa nani?
- Usiache siku yoyote ipite bila kupata chakula cha roho na nafsi yako kwa kuwa kipo wakati wote kwa ajili yako.
Mungu mwenyewe aliyetuita ni mwaminifu, naye atafanya katika Jina la Mwana wake Mpendwa Yesu Kristo, Bwana na Mwokozi wa maisha yetu. Amen
‘Utupe leo riziki yetu’
Isaack Zake
Wakili, Mwalimu na Mshauri
Isaack Zake ni wakili wa kujitegemea na mshauri katika masuala mbalimbali ya sheria za kazi na rasilimali watu, ndoa na sheria za ardhi na mikataba. Isaack Zake ni mwanzilishi wa mtandao wa kutoa elimu, ushauri na msaada wa kisheria wa www.ulizasheria.co.tz ni mwandishi wa vitabu na makala mbalimbali kwenye nyanja za kisheria, kijamii, kiuchumi na kiroho na mwalimu wa makundi mbalimbali ya kijamii kupitia mtandao wa www.isaackzake.co.tz . Isaack Zake pia ni Mkurugenzi wa Idara ya Sheria na Uhusiano wa chama cha Waajiri TAACIME – www.taacime.co.tz.
Wasiliana na Isaack Zake kwa barua pepe info@isaackzake.co.tz au kwa simu 0713 888 040 kwa ushauri na mafundisho. Mungu akubariki sana.
Leave a Reply
Want to join the discussion?Feel free to contribute!