Day.14. Spiritual Food: Imani kwa Yesu na utendaji wa kazi za Mungu – 2

Utangulizi
Karibu sana ndugu yangu msomaji wa mtandao huu wa isaack zake. Katika kipengele cha maarifa ya kiroho ya Uliza Neno tunakwenda kujifunza mambo mbalimbali yanayoanishwa na neno la Mungu kwa lengo la kutusaidia utu wetu katika safari na majukumu tuliyonayo hapa duniani siku kwa siku. Katika somo lililopita tuliendelea kujifunza habari za kusudi la chakula. Makala iliyopita tunazungumzia uhusiano wa imani kwa Yesu na utendaji wa kazi za Mungu. Leo tunaendelea zaidi juu ya uhusiano huo.Karibu sana.
‘Yesu akajibu, akawaambia, Hii ndio kazi ya Mungu, mwaminini yeye aliyetumwa na yeye’ Yn.6:29
Maneno haya aliyasema Bwana Yesu ajibu swali la makutano ambalo waliuliza juu ya utendaji wa kazi za Mungu.
Mambo ya kujifunza
- Imani katika Kristo ndiyo inatuwezesha kuzitenda kazi za Mungu. Hii ina maana kukaa ndani ya Kristo na kufuata maelekezo yake ndio njia pekee ya kushiriki kazi za Mungu. Ni lazima kufahamu hakuna mtu awezaye kujitwalia mamlaka ya kufanya kazi ya Mungu pasipo kutumwa na Mungu.
- Yesu Kristo ndiye Kichwa cha Kanisa na Kanisa ndio mwili wake, maelekezo yote juu ya utendaji wa viungo vya mwili hutoka kwenye Kichwa ambaye ni Kristo. Kanisa ambalo ni mwili wake ni lazima lifanye kazi kulingana na maelekezo ya Kristo mwenyewe.
- Wapo watu wajiingizao kushawishi watu kutokana na maneno au miujiza inayoonekana katika utendaji wao lakini si watendaji kazi na Mungu. Usitishike na ushawishi wa maneno au miujiza tafuta neno angalia mtu huyo imani yake na maelekezo anayotoa yanakupeleka kwa Yesu au kwa huyo mtu binafsi.
- Maelekezo, mahubiri, ishara, miujiza yote isiyotoka kwa Bwana Yesu si kazi za Mungu hizo ni za kibinadamu na yule mwovu. Hakikisha maelekezo na ishara zinakuongezea uhusiano wako binafsi na Mungu zaidi ya ule unaojenga na mtumishi au muhubiri.
- Bwana Yesu alishasema si kila mtu amwitaye Bwana Bwana ataurithi uzima wa milele ila wale wayafanyao mapenzi yake. Tumwombe Bwana Yesu kwa neema yake atupe chakula cha kutusaidia kukuza imani yetu kwa kiwango cha kutenda kazi za Mungu kila siku.
Mungu mwenyewe aliyetuita ni mwaminifu, naye atafanya katika Jina la Mwana wake Mpendwa Yesu Kristo, Bwana na Mwokozi wa maisha yetu. Amen
‘Utupe leo riziki yetu’
Isaack Zake
Wakili, Mwalimu na Mshauri
Isaack Zake ni wakili wa kujitegemea na mshauri katika masuala mbalimbali ya sheria za kazi na rasilimali watu, ndoa na sheria za ardhi na mikataba. Isaack Zake ni mwanzilishi wa mtandao wa kutoa elimu, ushauri na msaada wa kisheria wa www.ulizasheria.co.tz ni mwandishi wa vitabu na makala mbalimbali kwenye nyanja za kisheria, kijamii, kiuchumi na kiroho na mwalimu wa makundi mbalimbali ya kijamii kupitia mtandao wa www.isaackzake.co.tz . Isaack Zake pia ni Mkurugenzi wa Idara ya Sheria na Uhusiano wa chama cha Waajiri TAACIME – www.taacime.co.tz.
Wasiliana na Isaack Zake kwa barua pepe info@isaackzake.co.tz au kwa simu 0713 888 040 kwa ushauri na mafundisho. Mungu akubariki sana.
Leave a Reply
Want to join the discussion?Feel free to contribute!