
Utangulizi
Karibu sana ndugu yangu msomaji wa mtandao huu wa isaack zake. Katika kipengele cha maarifa ya kiroho ya Uliza Neno tunakwenda kujifunza mambo mbalimbali yanayoanishwa na neno la Mungu kwa lengo la kutusaidia utu wetu katika safari na majukumu tuliyonayo hapa duniani siku kwa siku. Katika somo lililopita tuliendelea kujifunza habari za kusudi la chakula. Makala iliyopita tulijifunza juu ya uwepo wa chakula cha Uzima kwa ajili yako.leo tunajiuliza swali la ‘Nani anakupa chakula cha kiroho? Karibu sana.
‘Msikitendee kazi chakula chenye kuharibika, bali chakula kidumucho hata uzima wa milele; ambacho Mwana wa Adamu atawapa, kwa sababu uyo ndiye alitiwa muhuri na Baba yaani Mungu’ Yn.6:27
Tunandelea kujifunza juu ya ujumbe wa Bwana Yesu kuhusu kupewa chakula cha kiroho.
Mambo ya kujifunza
- Nyakati hizi tunapata mahubiri ya neno kupitia vyombo vingi sana tofauti na kuudhuria kanisani pekee kama miaka 20 iliyopita. Kwa sasa kuna radio, Tv, mitandao ya kijamii, mikutano mbalimbali ya injili, semina n.k
- Wahubiri wamekuwa wengi sana kiasi kwamba watu wengine wanashindwa kujua ni yapi mafundisho sahihi. Wengine wanaamini sana watu kuliko neno linalohubiriwa, na wapo walio wengi waliojiingiza kwa maslahi yao wasihubiri injili ya kweli.
- Bwana Yesu anatueleza kupitia andiko hili ya kuwa ni Mwana wa Adamu pekee aliyetiwa muhuri na Baba yaani Mungu kuwapa wanadamu chakula cha kiroho. Hivi ndivyo maandiko yanavyosema.
- Mtu wa Mungu usitarajie chakula cha kiroho kutoka kwa mwanadamu, bila kujali karama au uwezo na ishara alizopewa mwanadamu, ni lazima kusikiliza maneno yanayotoka kinywani mwake kwa taadhari. Tuna kila sababu ya kuchunguza mafundisho tunayopokea kila siku.
- Usiweke imani kwa mtu kwani inawezekana neno linalotoka kinywani kwake si CHAKULA kwako. Mwombe Mungu katika Jina la Yesu akuongoze mahali au eneo ambalo utapata chakula chako cha kila siku.
- Usiweke imani yako kwa mtu kwani ni Yesu pekee anayejua ‘diet’ yako kwa siku ya leo. Haimaanishi ukatae kila neno linalotoka kwa mtumishi au ukubali kila neno ila muhimu kwako Mungu ampe kibali yule aliyepewa neno ‘chakula’ chako kwa siku ya leo.
- Pia jiwekee utaratibu wa kujifunza wewe binafsi maandiko kwani yapo ambayo Mungu anataka kukusemesha wewe binafsi si lazima apitie kwa mtu mwengine.
Mungu mwenyewe aliyetuita ni mwaminifu, naye atafanya katika Jina la Mwana wake Mpendwa Yesu Kristo, Bwana na Mwokozi wa maisha yetu. Amen
‘Utupe leo riziki yetu’
Isaack Zake
Wakili, Mwalimu na Mshauri
Isaack Zake ni wakili wa kujitegemea na mshauri katika masuala mbalimbali ya sheria za kazi na rasilimali watu, ndoa na sheria za ardhi na mikataba. Isaack Zake ni mwanzilishi wa mtandao wa kutoa elimu, ushauri na msaada wa kisheria wa www.ulizasheria.co.tz ni mwandishi wa vitabu na makala mbalimbali kwenye nyanja za kisheria, kijamii, kiuchumi na kiroho na mwalimu wa makundi mbalimbali ya kijamii kupitia mtandao wa www.isaackzake.co.tz . Isaack Zake pia ni Mkurugenzi wa Idara ya Sheria na Uhusiano wa chama cha Waajiri TAACIME – www.taacime.co.tz.
Wasiliana na Isaack Zake kwa barua pepe info@isaackzake.co.tz au kwa simu 0713 888 040 kwa ushauri na mafundisho. Mungu akubariki sana.
Leave a Reply
Want to join the discussion?Feel free to contribute!