
Utangulizi
Karibu sana ndugu yangu msomaji wa mtandao huu wa isaack zake. Katika kipengele cha maarifa ya kiroho ya Uliza Neno tunakwenda kujifunza mambo mbalimbali yanayoanishwa na neno la Mungu kwa lengo la kutusaidia utu wetu katika safari na majukumu tuliyonayo hapa duniani siku kwa siku. Katika somo lililopita tuliendelea kujifunza habari za kusudi la chakula. Makala iliyopita kujiuliza swali la ‘Je, ni chakula gani kinakushughulisha?. Leo tunaendelea kujifunza juu ya uwepo wa chakula cha Uzima kwa ajili yako. Karibu sana.
‘Msikitendee kazi chakula chenye kuharibika, bali chakula kidumucho hata uzima wa milele; ambacho Mwana wa Adamu atawapa, kwa sababu uyo ndiye alitiwa muhuri na Baba yaani Mungu’ Yn.6:27
Tunandelea kujifunza juu ya ujumbe wa Bwana Yesu kwa wanafunzi wake kuhusiana na aina za chakula na kipaombele wanachopaswa kuwa nacho katika ulaji.
Mambo ya kujifunza
- Mpaka sasa tunafahamu juu ya uwepo wa aina za chakula yaani kile chakula cha utu wa nje yaani mwili na chakula cha utu wa ndani yaani roho na nafsi.
- Bwana Yesu anatuonesha juu ya matokeo ya kila aina ya chakula, ya kwamba kile ambacho tunakitafuta kwa ajili ya miili yetu, mwisho wake ni uharibifu, lakini kile ambacho ni chakula kwa ajili ya roho na nafsi zetu mwisho wake ni uzima.
- Kwa maneno haya tunapata mtazamo mpya juu ya kuendesha maisha yetu na kufanya uchaguzi sahihi kila siku hasa kuhusu ulaji wetu. Ni lazima tufahamu ya kuwa roho na nafsi zetu zinahitaji chakula kila siku kama ilivyo miili yetu.
- Ili roho na nafsi zetu ziweze kudumu milele katika hali ya uzima hata pasipo mwili ni lazima tujenge utamaduni wa kutafuta chakula cha kurutubisha roho na nafsi kuliko hata tunavyotafuta kile cha miili yetu.
- Chakula cha kiroho kinapaswa kuwa kipaombele chetu cha kwanza kila tunapopata nafasi ya kuamka asubuhi kila siku. Tunafahamu ili tuweze kutenda kazi za Mungu na kutimiza makusudi yake katika majira au muda tulionao, ni lazima tule kiroho kila siku.
- Bwana Yesu ametuwekea nafasi na neema ya kujua juu ya uwepo wa chakula cha kiroho, suala la uamuzi sahihi na utashi wa kukitafuta chakula hicho ni la kila mtu binafsi.
Mungu mwenyewe aliyetuita ni mwaminifu, naye atafanya katika Jina la Mwana wake Mpendwa Yesu Kristo, Bwana na Mwokozi wa maisha yetu. Amen
‘Utupe leo riziki yetu’
Isaack Zake
Wakili, Mwalimu na Mshauri
Isaack Zake ni wakili wa kujitegemea na mshauri katika masuala mbalimbali ya sheria za kazi na rasilimali watu, ndoa na sheria za ardhi na mikataba. Isaack Zake ni mwanzilishi wa mtandao wa kutoa elimu, ushauri na msaada wa kisheria wa www.ulizasheria.co.tz ni mwandishi wa vitabu na makala mbalimbali kwenye nyanja za kisheria, kijamii, kiuchumi na kiroho na mwalimu wa makundi mbalimbali ya kijamii kupitia mtandao wa www.isaackzake.co.tz . Isaack Zake pia ni Mkurugenzi wa Idara ya Sheria na Uhusiano wa chama cha Waajiri TAACIME – www.taacime.co.tz.
Wasiliana na Isaack Zake kwa barua pepe info@isaackzake.co.tz au kwa simu 0713 888 040 kwa ushauri na mafundisho. Mungu akubariki sana.
Leave a Reply
Want to join the discussion?Feel free to contribute!