
Utangulizi
Karibu sana ndugu yangu katika mafunzo juu ya Kipawa/Vipawa katika ukurasa huu wa vipaji. Katika makala zilizopita tumekuwa tukangalia juu ya misingi 4 ya kipaji. Leo tunakwenda kujuliza swali ya kuwa unapa nini dunia leo? Karibu sana tujifunze.
Dunia kwa sasa ina watu takribani Bilioni 7.7, hii ni idadi kubwa sana ya watu na kwamba watu wote hawa kila mmoja ana kipawa cha aina yake. Kipaji cha kila mmoja hakifanani na mwengine ingawa majukumu au namna ya matumizi ya kipaji yanaweza kufanana. Hii ina maana unaweza kuwa mwanamuziki lakini aina ya muziki unaotakiwa kufanya haupaswi kufanana na mwengine.
Maisha yetu ya kila siku yanashibishwa na kazi za vipawa za watu wengine kila siku. Tunatembea kwenye vyombo vya usafiri, tunakaa katika nyumba nzuri zimejengwa kwa ustadi, tunapata mwangaza kupitia umeme, tuna vyombo vya mawasiliano n.k zote hizi ni kazi za watu ambao wametumia elimu zao na vipaji vyao kusababisha maisha yetu kuwa bora zaidi.
Wewe na mimi tunavyo vitu ambavyo havipo kwa wengine. Pata picha dunia nzima wewe au mimi tunacho kitu ambacho hakipatikani kwa mwengine yeyote, je ni kwa kiasi gani tunaweza kutumia kitu hicho kuzalisha thamani kuu siku ya leo. Wengi tunadharau kipawa tulichonacho, hatuijui thamani yake kwa dunia, muhimu sana siku ya leo kukinoa kipaji chetu na kuathiri ulimwengu wetu kwa njia chanya na kuleta mabadiliko yanayostahili. Unacho kitu cha kuipa dunia siku ya leo, ili dunia nayo inijaze na vitu kwa kipimo kikubwa sana.
Weka kipaji chako kazini siku ya leo ili dunia inufaike nawe utanufaika na kupata nafasi yako duniani.
Fanya mabadiliko makubwa katika kuboresha maisha ya wengine kwa kufanyia kazi kipaji chako kila siku. Wapo watu wengi wanakusubiri wewe uingie kazini katika kutumia kipaji chako.
‘Kipaji changu, fursa yangu’
Isaack Zake
Wakili, Mwalimu na Mshauri
Wasiliana na Isaack Zake kwa barua pepe info@isaackzake.co.tz au kwa simu 0713 888 040 kwa ushauri na mafundisho. Mungu akubariki sana.
Leave a Reply
Want to join the discussion?Feel free to contribute!