• Twitter
  • Facebook
  • Instagram
Isaack Zake
  • Home
  • Kuhusu Mimi
  • Huduma
  • Vitabu
  • ULIZA
  • Shop
  • Blog
  • Mawasiliano
  • Search
  • Menu Menu
SPIRITUAL FOOD

Day.18. Spiritual Food: Je, unapata Chakula cha Kweli?

Utangulizi

Karibu sana ndugu yangu msomaji wa mtandao huu wa isaack zake. Katika kipengele cha maarifa ya kiroho ya Uliza Neno tunakwenda kujifunza mambo mbalimbali yanayoanishwa na neno la Mungu kwa lengo la kutusaidia utu wetu katika safari na majukumu tuliyonayo hapa duniani siku kwa siku. Katika somo lililopita  tuliendelea kujifunza habari za kusudi la chakula. Makala iliyopita tuliangalia juu ya kuwekaimani kwa Mungu si kwa mwanadamu. Leo tunaangalia kuhusu Chakula cha Kweli.Karibu sana.

‘Yesu akawaambia, Amin, amin, nawaambieni, Siye Musa aliyewapa chakula kile cha mbinguni, bali Baba yangu anawapa ninyi chakula cha kweli kitokacho mbinguni’ Yn.6:32

Mambo ya kujifunza

  • Safari ya wana wa Israel kutoka Misri kwenda Kanaani ni mfano wa safari ya Kanisa lililokombolewa katika Agano Jipya. Tunaweza kujifunza mengi sana kupitia safari hii ya wana wa Israel.

  • Kama walivyokuwa wana wa Israel walivyopita vipindi mbalimbali yaani kutoka utumwani  kwenda Jangwani na kisha Kanaani, hali kadhalika Kanisa nalo linapita vipindi hivyo vya kutoka utumwani hali ya utumwa wa dhambi, kupita jangwani hapa ni kipindi cha mpito kukua kiroho na hatimaye kuingia au kuziishi baraka za ufalme wa Mungu kama Kanaani.

  • Tunajifunza ya kuwa maisha ya Jangwani wana wa Israel waliishi kwa kula MANA katika kipindi cha miaka 40. Mana hii ilitoka mbinguni kila siku ambapo walipaswa kuokota asubuhi. Kadhalika na sisi katika safari yetu ya kumjua Mungu tunahitaji chakula cha kweli au MANA kutoka kwa Bwana Yesu kila siku.

  • Kama vile Mungu alivyohakikisha ya kuwa mana ipo kila siku bila kujali hali ya uasi au kiroho ya wana wa Israel vivyo hivyo anatuhakikishia KILA SIKU uwepo wa chakula cha kiroho kwa ajili yako na yangu kutoka kwa Bwana Yesu. Ndio maana andiko linasema ‘…bali Baba yangu anawapa ninyi chakula cha kweli kitokacho mbinguni’ neno anawapa ni mwendelezo au kitendo kinachoendelea kila siku.

  • Wakristo wanapaswa kuwa waangalifu hasa katika nyakati hizi, kutokana na uwepo wa manabii wa uongo ambao hawatoi chakula cha kweli bali wanatafuta maslahi yao, hivyo kuwafanya watoto wa Mungu kudumaa kiroho na kukaa muda mrefu Jangwani.

  • Ukitaka kupima endapo neno unalosikia kama ni chakula cha kiroho au la angalia endapo uhusiano wako na Yesu unaimarika kila siku au unadhoofika. Ikiwa chakula unachopata ni cha kiroho kweli hicho kitakujengea hamu ya kufanya mapenzi ya Mungu na kumtumikia kila siku. Ikiwa neno unalosikia bila kujali ni muhubiri gani au ana sifa gani lakini halikusaidii kuimarisha uhusiano wako na Mungu bali maneno yanayokusukuma kupata vitu au mahitaji tu ya hapa duniani basi kuna changamoto katika ulaji wako.

Mungu mwenyewe aliyetuita ni mwaminifu, naye atafanya katika Jina la Mwana wake Mpendwa Yesu Kristo, Bwana na Mwokozi wa maisha yetu. Amen

‘Utupe leo riziki yetu’

Isaack Zake

Wakili, Mwalimu na Mshauri

Isaack Zake ni wakili wa kujitegemea na mshauri katika masuala mbalimbali ya sheria za kazi na rasilimali watu, ndoa na sheria za ardhi na mikataba. Isaack Zake ni mwanzilishi wa mtandao wa kutoa elimu, ushauri na msaada wa kisheria wa www.ulizasheria.co.tz ni mwandishi wa vitabu na makala mbalimbali kwenye nyanja za kisheria, kijamii, kiuchumi na kiroho na mwalimu wa makundi mbalimbali ya kijamii kupitia mtandao wa www.isaackzake.co.tz . Isaack Zake pia ni Mkurugenzi wa Idara ya Sheria na Uhusiano wa chama cha Waajiri TAACIME – www.taacime.co.tz.

Wasiliana na Isaack Zake kwa barua pepe info@isaackzake.co.tz au kwa simu 0713 888 040 kwa ushauri na mafundisho. Mungu akubariki sana.

Share this:

  • Click to share on LinkedIn (Opens in new window) LinkedIn
  • Click to share on X (Opens in new window) X
  • Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
  • Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
  • Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
May 16, 2020/0 Comments/by Isaack Zake
Share this entry
  • Share on Facebook
  • Share on Twitter
  • Share on WhatsApp
  • Share on LinkedIn
  • Share by Mail
https://isaackzake.co.tz/wp-content/uploads/2020/02/zake-2.png 0 0 Isaack Zake https://isaackzake.co.tz/wp-content/uploads/2020/02/zake-2.png Isaack Zake2020-05-16 01:00:002020-05-15 23:22:55Day.18. Spiritual Food: Je, unapata Chakula cha Kweli?
0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

MAKUNDI YA MAKALA

  • ELIMU (20)
  • FAMILIA (2)
  • KIPAJI CHANGU (14)
  • KUSUDI LA MAISHA (13)
  • MAANA YA KAZI (17)
  • MAKALA (2)
  • NENO LA MUNGU (8)
  • SPIRITUAL FOOD (55)

MAKALA MPYA

  • Day.55. Spiritual Food: Je, ulipo kuna maneno ya uzima wa milele? March 26, 2022
  • Day.54. Spiritual Food: Je, unataka kuondoka? March 24, 2022
  • Day.53. Spiritual Food: Je umekwazwa na kitu gani maishani? January 15, 2022
  • AES.20. Upimaji ni rahisi kuwa na udanganyifu November 8, 2021
  • Day.52. Spiritual Food: Twamwendea Bwana Yesu kwa Neema October 18, 2021

Kuhusu | Vitabu | Mawasiliano

© 2020 Isaack Zake. All Rights Reserved

Day.17. Spiritual Food: Weka imani kwa Mungu si mwanadamu Day.19. Spiritual Food: Kipo chakula kwa ajili yako leo
Scroll to top