
Utangulizi
Karibu sana ndugu yangu msomaji wa mtandao huu wa isaack zake. Katika kipengele cha Chakula cha kiroho. Makala iliyopita tunazungumzia uhusiano wa imani kwa Yesu na utendaji wa kazi za Mungu. Leo tunaangalia uhusiano wa imani na ishara. Karibu sana.
‘wakamwambia, Unafanya ishara gani basi, ili tuone tukuamini? Unatenda kazi gani?’ Yn.6:30
Maneno haya aliyasema Bwana Yesu ajibu swali la makutano ambalo waliuliza juu ya utendaji wa kazi za Mungu.
Mambo ya kujifunza
- Wanadamu siku zote ni watu wa mashaka ambao ni vigumu mno kumwamini Mungu pasipo ishara. Ndio maana watu wengi hupotezwa kwa sababu ya kufuata ishara. Tunaona kwenye maandiko hata Musa alipoenda kuwatoa wana wa Israel kule Misri pamoja na ujumbe alipewa ishara za kuwatambulisha Mungu aliyemtuma.
- Katika nyakati hizi za mwisho Bwana Yesu alionya juu ya kizazi cha kuasi kinavyotaka kuishi kwa ishara. Alitoa maonyo kwa kizazi hiki juu ya kupotezwa kwa sababu ya ishara.
- Je, imani zetu tumezijenga katika ishara au neno la Kristo? Maandiko yanaeleza juu ya imani kuja kwa kusikia na kusikia huja kwa neno la Kristo. Ni muhimu sana kwetu kuzijenga imani zetu katika neno la Kristo.
- Je, kabla hujavutwa na ishara iliyofanyika kwako au kwa jirani yako unajiuliza juu ya neno la Mungu analokusemesha? Watu wengi hufuata miujiza na ishara ambazo mwisho wa siku huaribu hali zao za kiroho na kuzalisha chuki dhidi ya wanafamilia, ndugu, jamaa na marafiki.
- Kila wakati tunapaswa kujenga imani yetu kutokana na neno ambalo Bwana Yesu Kristo anatusemesha kupitia vyanzo mbalimbali na si matendo ya miujiza ambayo wapo wengi wanaoweza kufanya lakini wasiwe wanamwakilisha Bwana Yesu. Haijalishi hata kama wanataja jina la Yesu muhimu kwako ni kuisikia sauti ya Mungu wewe binafsi ambayo inakuongoza. Ndio maana maandiko yanasisitiza umuhimu wa kujifunza binafsi juu ya habari za Mungu kwa kujenga uhusiano wako binafsi kila siku.
- Mungu anaweza kuzungumza na wewe kwa kutumia ishara au matendo ya miujiza kwa sababu zake lakini si mara zote hutumia utaratibu huo. Ila kwa wakati wote hulitumia neno lake ambalo lipo moyoni mwako kwa ajili ya kukuongoza.
Mungu mwenyewe aliyetuita ni mwaminifu, naye atafanya katika Jina la Mwana wake Mpendwa Yesu Kristo, Bwana na Mwokozi wa maisha yetu. Amen
‘Utupe leo riziki yetu’
Isaack Zake
Wakili, Mwalimu na Mshauri
Isaack Zake ni wakili wa kujitegemea na mshauri katika masuala mbalimbali ya sheria za kazi na rasilimali watu, ndoa na sheria za ardhi na mikataba. Isaack Zake ni mwanzilishi wa mtandao wa kutoa elimu, ushauri na msaada wa kisheria wa www.ulizasheria.co.tz ni mwandishi wa vitabu na makala mbalimbali kwenye nyanja za kisheria, kijamii, kiuchumi na kiroho na mwalimu wa makundi mbalimbali ya kijamii kupitia mtandao wa www.isaackzake.co.tz . Isaack Zake pia ni Mkurugenzi wa Idara ya Sheria na Uhusiano wa chama cha Waajiri TAACIME – www.taacime.co.tz.
Wasiliana na Isaack Zake kwa barua pepe info@isaackzake.co.tz au kwa simu 0713 888 040 kwa ushauri na mafundisho. Mungu akubariki sana.
Leave a Reply
Want to join the discussion?Feel free to contribute!