• Twitter
  • Facebook
  • Instagram
Isaack Zake
  • Home
  • Kuhusu Mimi
  • Huduma
  • Vitabu
  • ULIZA
  • Shop
  • Blog
  • Mawasiliano
  • Search
  • Menu Menu
SPIRITUAL FOOD

Day.8. Spiritual Food: Gharama ya chakula cha kiroho

Utangulizi

Karibu sana ndugu yangu msomaji wa mtandao huu wa isaack zake. Katika kipengele cha maarifa ya kiroho ya Uliza Neno tunakwenda kujifunza mambo mbalimbali yanayoanishwa na neno la Mungu kwa lengo la kutusaidia utu wetu katika safari na majukumu tuliyonayo hapa duniani siku kwa siku. Katika somo lililopita  tuliendelea kujifunza habari za kusudi la chakula. Makala iliyopita tulijifunza habari za kipaombele cha kulisha utu wa ndani. Leo tunaangalia juu ya Gharama ya Chakula cha kiroho. Karibu sana.

 ‘Haya, kila aonaye kiu, njoni majini, Naye asiye na fedha; njoni, nunueni mle; Naam, njoni, nunueni divai na maziwa, bila fedha na bila thamani’ Isa.55:1

Ujumbe huu ulionenwa na Nabii Isaya ni ujumbe muhimu wa kuwaalika watu kwa ajili ya kupata chakula cha kiroho bure. Kuna mambo ya kujifunza juu ya ujumbe huu.

Mambo ya kujifunza

  • Sisi zote tunajua ya kwamba chakula chochote ni gharama wala hakuna chakula cha bure. Hata kama leo umekula chakula cha bure nyumbani lakini yupo mtu aliyeingia gharama kukileta chakula hicho.

  • Moja ya hitaji la msingi kabisa katika maisha ya mwanadamu ni kupata mlo wa kila siku. Mtu atakuwa tayari kukosa malazi au mavazi lakini si chakula. Kila mmoja wetu anahitaji chakula.

  • Kwa kuwa na chakula ni gharama, je vipi kuhusu upatikanaji wa chakula cha kiroho.Hatununui chakula cha kiroho kwa fedha wala kwa kitu chochote cha thamani bali tunahitaji kuwa na KIU na NJAA ya chakula cha kiroho. Kama ilivyo kwa chakula cha kimwili ili kukipata tunahitaji fedha, lakini kwa chakula cha kiroho tunahitaji kiu na njaa.

  • Msingi wa kupata chakula cha kiroho ni hali ya uhitaji wako wa ndani yaani Kiu na Njaa ya kiroho. Hatupati leo chakula kwa sababu hatujatengeneza kiu na njaa ya kutosha ndani yetu. Hali ya kukosa kiu na njaa ya chakula cha kiroho inatupelekea kutokuwa na msukumo wa kukitafuta chakula hicho.

  • Bwana Yesu alipoanza kuhubiri alianza na ‘heri walio masikini wa roho..’ yaani wamebarikiwa wenye uhitaji wa mambo ya rohoni maana ufalme wa Mungu ni wao. Ukijua umuhimu/kusudi la chakula kwenye maisha yako kwamba ni kutunza uhai na kukuwezesha kufanya kazi ni wazi utaweka kipaombele kwa kutafuta neno au chakula kwa ajili ya nafsi na roho yako kila siku.

  • Jenga kiu na njaa ya chakula cha kiroho kila siku ndio gharama ya kukipata kila siku. Tuanze sasa maadam ipo leo kwa kumwendea Bwana Yesu kwa moyo wa kiu na njaa ya chakula cha kiroho ili atushibishe kila siku.

Mungu mwenyewe aliyetuita ni mwaminifu, naye atafanya katika Jina la Mwana wake Mpendwa Yesu Kristo, Bwana na Mwokozi wa maisha yetu. Amen

‘Utupe leo riziki yetu’

Isaack Zake

Wakili, Mwalimu na Mshauri

Isaack Zake ni wakili wa kujitegemea na mshauri katika masuala mbalimbali ya sheria za kazi na rasilimali watu, ndoa na sheria za ardhi na mikataba. Isaack Zake ni mwanzilishi wa mtandao wa kutoa elimu, ushauri na msaada wa kisheria wa www.ulizasheria.co.tz ni mwandishi wa vitabu na makala mbalimbali kwenye nyanja za kisheria, kijamii, kiuchumi na kiroho na mwalimu wa makundi mbalimbali ya kijamii kupitia mtandao wa www.isaackzake.co.tz . Isaack Zake pia ni Mkurugenzi wa Idara ya Sheria na Uhusiano wa chama cha Waajiri TAACIME – www.taacime.co.tz.

Wasiliana na Isaack Zake kwa barua pepe info@isaackzake.co.tz au kwa simu 0713 888 040 kwa ushauri na mafundisho. Mungu akubariki sana.

Share this:

  • Click to share on LinkedIn (Opens in new window) LinkedIn
  • Click to share on X (Opens in new window) X
  • Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
  • Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
  • Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
April 10, 2020/0 Comments/by Isaack Zake
Share this entry
  • Share on Facebook
  • Share on Twitter
  • Share on WhatsApp
  • Share on LinkedIn
  • Share by Mail
https://isaackzake.co.tz/wp-content/uploads/2020/02/zake-2.png 0 0 Isaack Zake https://isaackzake.co.tz/wp-content/uploads/2020/02/zake-2.png Isaack Zake2020-04-10 05:39:392020-04-10 05:39:45Day.8. Spiritual Food: Gharama ya chakula cha kiroho
0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

MAKUNDI YA MAKALA

  • ELIMU (20)
  • FAMILIA (2)
  • KIPAJI CHANGU (14)
  • KUSUDI LA MAISHA (13)
  • MAANA YA KAZI (17)
  • MAKALA (2)
  • NENO LA MUNGU (8)
  • SPIRITUAL FOOD (55)

MAKALA MPYA

  • Day.55. Spiritual Food: Je, ulipo kuna maneno ya uzima wa milele? March 26, 2022
  • Day.54. Spiritual Food: Je, unataka kuondoka? March 24, 2022
  • Day.53. Spiritual Food: Je umekwazwa na kitu gani maishani? January 15, 2022
  • AES.20. Upimaji ni rahisi kuwa na udanganyifu November 8, 2021
  • Day.52. Spiritual Food: Twamwendea Bwana Yesu kwa Neema October 18, 2021

Kuhusu | Vitabu | Mawasiliano

© 2020 Isaack Zake. All Rights Reserved

AES.6. Changamoto za Mfumo rasmi wa Elimu Kipaji.1. Maana ya Kipaji
Scroll to top